Jumanne, 24 Januari 2017

MKRISTO AMKA TOKA USINGIZINI VOL..3

πŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”Ί
MKRISTO AMKA TOKA USINGIZINI
 MKRISTO WEWE NI BALOZI WA UFALME WA MBINGUNI HUMU DUNIANI
 Baba Mungu nakushukuru kwaajili ya huyu mpendwa wako anaye fuatilia masomo haya naomba yale yaliyo makusudi yako kwenye hili somo naomba yaweze kutimia juu yake. Tazama umetuweka sisi wanadamu hapa duniani ili tukutumikie wewe na ili tuliheshimu jina lako. pia umetuweka sisi wanadamu hapa Duniani ili kuvitiisha viumbe wote wa kila aina. Ee Mwenyezi Mungu mpe kila asomaye masomo haya uwezo wa kujitambua yeye ni nani na nafasi yake katika kutimiza yaliyo mapenzi yako kwa ulimwengu huu. AMEN
 πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»

Huu ni mwendelezo wa somo letu hili linalomkumbusha Mkristo wajibu wake na nafasi yake katika kutimiza mapenzi ya Mungu kwa ulimwengu huu.
katika mwendelezo huu nitazungumzia kuhusu Mtazamo wa Mungu juu yako ewe mkristo, hasa nafasi yako katika ulimwengu huu.
➤Mkristo ni Balozi wa Ufalme wa Mungu katika Ulimwengu huu.
 Ni hakika kwamba Mkristo ni Balozi wa Ufalme wa Mungu humu duniani. Maana ya balozi ndiyo hii; Balozi ni mwakilishi wa nchi yake katika nchi nyingine ya ugenini. Neno "Balozi" kwa kingereza ni "Ambassador" lenye maana kama hiyo hiyo niliyoitoa ya balozi ambayo inasema 'ambasssdor is a minister of the highest rank sent to a foreign court to represent there his sovereign or country. Sometimes called ambassador-in-residence (http://wikitionary.org). Hivyo tunapozungumza kuhusu Mkristo wewe ni balozi wa Ufalme wa Mungu hapa Duniani tunamaanisha:
➽Mwakilishi wa Ufalme wa Mungu. (Representative of Kingdom of God)
➽ Mtu uliyeaminiwa na Mungu
➽ Mtu uliyepewa uwezo na Mungu wa kuweza kumwakilisha hapa Duniani
➽ Umepewa wajibu na Mungu unapaswa kuutimiza (Mt.10:8)
➽ Mtu mwenye sifa zote na vigezo vyote vya kuwa mfano wa Mungu (Mwa.1:27)
➽ Mungu anakutegemea sana katika kutenda mambo yake hapa Duniani
➽ Muda wako wa kuwepo hapa duniani umehesabiwa (Hutaishi milele katika ulimwengu huu hivyo tumia muda wako vizuri)
➽Wewe sio wa Ulimwengu huu bali ni wa Ufalme wa Mungu (Hivyo ishi ukitambua hapa sio kwenu, kwenu ni mbinguni. Dunia isikufanye ukasahau kwenu) Japo tunaishi ulimwenguni humu kwa namna ya kwimwili lakini una wito ulioitiwa kufanyana kwa muda maalumu, muda ukiisha utatoa hesabu.
➽ Unapaswa kutenda yale ambayo Mungu amekuagiza kuyatenda na sio kutenda mambo ya ulimwengu huu.
➽ Ishi ukitambua kwamba Mungu ndiye atakaye kulipa kwa yale yote utakayo yatenda na sio ulimwengu huu (matendo maovu na matendo mema yote yana malipo yake huko mbinguni. Mungu aliye mwajiri wako amekwisha kukupa)
➽Usitende jambo kwa kuwaangalia wanadamu wanasema nini bali Mungu anasema nini.
➽Tambua kwamba msaada juu ya kila unachokitenda haupatikani popote pale ila kwa Mungu pekee aliyekutuma.(usitafute msaada kwa wanadamu au kwa waganga au kwa miungu mingine)
➽Tambua kwamba mwajiri wako 'MUNGU' amekwisha kuandalia utaratibu mzima wa jinsi utakavyoish; chakula,malazi na makazi pia utaratibu wote wa maisha yako hapa duniani. Ndiyo maana anasema usisumukie kwamba utakula  nini au utakunywa nini.
➽Tambua kwamba unapaswa kuwasiliana na Mwajiri wako kila wakati ili kumfahamisha kila kinachoendelea na njia pekee ya mawasiliano ni 'MAOMBI' 
➽Tambua kwamba kuna mkataba ulioingia wewe na mwajiri wako, unapaswa uufate. 
➽Tambua kuna mambo ambayo mwajiri wako amekwambia uyafuate pindi uwapo humu duniani na unapaswa ufuate (AMRI KUMI)


⧫Ni wakati wa kujitathimini kwamba upo wapi. je! umelala au umeamka? Je! upo kazini kuitenda kazi ya Bwana aliyokuitia hapa ulimwenguni au la? 
⧫Katika  chapisho linalokuja 'VOL....04' Tutaona uchambuzi zaidi wa Mkristo kuwa Balozi wa Mungu hapa ulimwenguni. hii ni sawa na utangulizi tuu wa somo litakalokuja karibu ujiunge nami katika kuliandaa kwa njia ya maombi ili Mungu aliwezeshe likawe na mafanikio makubwa kwa kila atakayesoma.πŸ”œπŸ”œπŸ”œπŸ”œπŸ”œπŸ”œπŸ”œπŸ”œ

⭆Usiache kufuatilia masomo yaliyopita na masomo mbalimbali kwenye blog yangu hii. 
⭆Share kwa wengine nao wapate kusoma na kufaidika kama wewe sasa.
⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲MUNGU AKUBARIKI SANA  ⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲

Mwandishi. Melchizedek Pokeaeli
➧ Unaweza kuyapata masomo mengine sehemu hizi zifuatazo
➢ christiansforum1.blogspot.com
 Facebook: Joyful house in Jesus Christ
WhatsApp https://chat.whatsapp.com/CWsNX9vneY95rYMeuLNW9I
Twitter @johnsonpaulPAUL

Maoni 1 :

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    JibuFuta