Jumatano, 18 Januari 2017

WAKATI WA KUAMKA TOKA USINGIZINI ….Vol.02

πŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”ΊπŸ”Ί

 WAKATI WA KUAMKA TOKA USINGIZINI ….Vol.02
MKRISTO AMKA USINGIZINI SASA!!!!!
Ahsante Ee Yesu Kristo Kwa NEEMA yako juu ya kila ambaye ni Mkristo anayesoma chapisho hili. Sehemu hii ya pili ya chapisho hili. Ee Baba Mungu mjazie neema ya kudumu katika pendo lako na kuyatenda yale yote yaliyo mapenzi yako. Ni kweli kwamba kuna wengine wengi ambao bado hawajakata shauri la kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao lakini kupitia wapendwa hawa wachache; maisha yao yakawe mfano kwa wengine yakawe na ushawishi juu ya wengine ili wamkubali Yesu Kristo. Amen!!
πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»πŸ”»

Mpendwa nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo!!!

⭆Utangulizi
Mtu awapo usingizini maana yake ni kwamba hana anachokifanya kwaajili ya maaendeleo yake kimwili, kiakili na kiuchumi hata kiroho. Ndiyo maana Biblia inatuonya kwamba TUSIUPENDE usingizi maana usingizi ni chanzo cha Umaskini.  “Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho ysko kusinzia” Ewe mvivu utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulalala kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.” (Mithali 6:4;9-11)
 Usingizi wa Wakristo ni  ubinafsi walionao; kujiona wao pekee ndiyo wanaostahili kuurithi uzima na wengine hawastaili wala hawatakiwi kustahilishwa kupitia Toba. Wakristo wamelala na kujisahau katika ili dimbwi la ubinafsi na kujivuna. Mkristo akimwona Mtua anatenda dhambi basi humsema badala ya kumsaidia hii ni kinyume cha mapenzi ya Mungu. WOKOVU tumeupata bure na kwa neema tu tunapaswa kuutoa bure (Mathayo 10:8) “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure”.. Ni kusudi la Mungu kwamba ulimwengu wote uokolewe na sio kuangamizwa.
Namshukuru Mungu kwaajili ya Neno lake hili linalowahusu wakristo, Neno linalohusu maisha yao kwaujumla na jinsi wanavyopaswa kuenenda ili wakawe ushuhuda kwa wengine. Katika sehemu ya ya kwanza ya Somo hili tuliona mambo mengi ambayo Mungu anasema nasi na anatukumbusha kwanza ikiwa ni kuhusu Upendo wa Mungu juu ya ulimwengu na huruma yake ambao haukuhesabu makosa yetu bali katika wingi wa maovu yetu yeye alituhurumia na kumtoa mwanaye mpendwa Yesu Kristo ili aje ulimwenguni na kuteswa na kufa kwaajili yetu, pia nilizungumzia kuhusu maisha ya mkristo yanapaswa yamzalie Bwana matunda, matunda hayo ikiwa ni pamoja na kuwafanya wale wasiokoka kuweza kuokoka na hapa utakuwa umempendeza Mungu kwa sababu ndiyo kusudi la Yesu Kristo alipoujia ulimwengu, alikuja kwaajili ya waliopotea awaokoe na kuwatoa kwenye vifungo vya shetani.
Karibu tuendelee na sehemu hii ya pili ya somo hili, japo ni vyema ukasoma na sehemu ya kwanza ya somo hili itakusaidia. 
Wakati wa kuamka usingizini ndiyo sasa mkristo unapaswa kutambua Mungu anafanya kazi pamoja na  wanadamu. Ndiyo maana Neno la Mungu linatuambia kwamba maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu. Kusudi la Mungu juu ya ulimwengu sio kuuhukumu ulimwengu bali ni kuuokoa anatamani katika siku ya mwisho, siku ya hukumu basi asilimia kubwa iwe ni ya wanaoelekea uzima wa milele.  Yesu kristo aliwapa uwezo na mamlaka wale wakristo wa kwanza aliokuwa nao ili wakaiendeleze kazi aliyoianza ya kuhubiri abari njema za ufalme wa mbinguni, na kuwaponya walio wagonjwa na kuwafungua walio kwenye vifungo na kuwasaidia walio katika dhiki (Mathayo 10:1-16). Neno la Mungu linaonyesha nguvu waliopewa wale wanafunzi wa Yesu Kristo juu ya Pepo, na juu ya magonjwa.
     ➻ Mkristo wa sasa Mbona huyatendi haya? Je kuna wagonjwa wangapi katiika eneo ulipo? Je kuna wangapi wanaosumbuliwa na pepo katika eneo ulipo? Umechukua hatua gani ya kupambana na hali hiyo. Je! Uliwaombea au uliwapa msaada wowote? Tambua leo kwamba ile mamlaka Yesu Kristo aliyowapa wanafunzi wake ipo ndani yako wewe umwaminiye Kristo ni wajibu wako kusimama kwa uaminifu katika maombi ili Mungu awezeshe kile alichokipanda ndani yako kifanye kazi. Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure”.
    ➻ Unapoitenda kazi ya Mungu kikamilifu basi unautimiza ule mpango wa Mungu ndani yako juu ya ulimwengu na Mungu atakubariki maradufu.  Kusudi la Mungu ni kila goti lipigwe mbele zake na kila ulimi ukiri ya kwamba Mungu ndiye Mfalme juu ya Ulimwengu wote (Ufu.5:13). Ni wajibu wako kutambua sasa unakitu ambacho Mungu anatamani ukifanye popote ulipo kwaajili ya ufalme wa Mbinguni. Mkristo tambua ya kwamba wewe ni balozi wa Ufalme wa Mbinguni hapa Duniani na umepewa mamlaka ya kuyatenda mambo yote katika Jina la Yesu Kristo.

Fuatilia somo mwendelezo wa somo hili kwenye Blog hii hii  http://pokeaeli.blogspot.com au pata masomo mengine mengi kupitia blog hii christiansforum1.blogspot.com
  •        Facebook like page hii Joyful House in Jesus Christ
  •         WhatsApp: 0752513159   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni