MKRISTO AMKA TOKA USINGIZINI
MKRISTO WEWE NI BALOZI WA UFALME WA MBINGUNI HUMU DUNIANI
Baba Mungu nakushukuru kwaajili ya huyu mpendwa wako anaye fuatilia masomo haya naomba yale yaliyo makusudi yako kwenye hili somo naomba yaweze kutimia juu yake. Tazama umetuweka sisi wanadamu hapa duniani ili tukutumikie wewe na ili tuliheshimu jina lako. pia umetuweka sisi wanadamu hapa Duniani ili kuvitiisha viumbe wote wa kila aina. Ee Mwenyezi Mungu mpe kila asomaye masomo haya uwezo wa kujitambua yeye ni nani na nafasi yake katika kutimiza yaliyo mapenzi yako kwa ulimwengu huu. AMEN
π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»π»Huu ni mwendelezo wa somo letu hili linalomkumbusha Mkristo wajibu wake na nafasi yake katika kutimiza mapenzi ya Mungu kwa ulimwengu huu.
katika mwendelezo huu nitazungumzia kuhusu Mtazamo wa Mungu juu yako ewe mkristo, hasa nafasi yako katika ulimwengu huu.
➤Mkristo ni Balozi wa Ufalme wa Mungu katika Ulimwengu huu.
Ni hakika kwamba Mkristo ni Balozi wa Ufalme wa Mungu humu duniani. Maana ya balozi ndiyo hii; Balozi ni mwakilishi wa nchi yake katika nchi nyingine ya ugenini. Neno "Balozi" kwa kingereza ni "Ambassador" lenye maana kama hiyo hiyo niliyoitoa ya balozi ambayo inasema 'ambasssdor is a minister of the highest rank sent to a foreign court to represent there his sovereign or country. Sometimes called ambassador-in-residence (http://wikitionary.org). Hivyo tunapozungumza kuhusu Mkristo wewe ni balozi wa Ufalme wa Mungu hapa Duniani tunamaanisha:
➽Mwakilishi wa Ufalme wa Mungu. (Representative of Kingdom of God)
➽ Mtu uliyeaminiwa na Mungu
➽ Mtu uliyepewa uwezo na Mungu wa kuweza kumwakilisha hapa Duniani
➽ Umepewa wajibu na Mungu unapaswa kuutimiza (Mt.10:8)
➽ Mtu mwenye sifa zote na vigezo vyote vya kuwa mfano wa Mungu (Mwa.1:27)
➽ Mungu anakutegemea sana katika kutenda mambo yake hapa Duniani
➽ Muda wako wa kuwepo hapa duniani umehesabiwa (Hutaishi milele katika ulimwengu huu hivyo tumia muda wako vizuri)
➽Wewe sio wa Ulimwengu huu bali ni wa Ufalme wa Mungu (Hivyo ishi ukitambua hapa sio kwenu, kwenu ni mbinguni. Dunia isikufanye ukasahau kwenu) Japo tunaishi ulimwenguni humu kwa namna ya kwimwili lakini una wito ulioitiwa kufanyana kwa muda maalumu, muda ukiisha utatoa hesabu.
➽ Unapaswa kutenda yale ambayo Mungu amekuagiza kuyatenda na sio kutenda mambo ya ulimwengu huu.
➽ Ishi ukitambua kwamba Mungu ndiye atakaye kulipa kwa yale yote utakayo yatenda na sio ulimwengu huu (matendo maovu na matendo mema yote yana malipo yake huko mbinguni. Mungu aliye mwajiri wako amekwisha kukupa)
➽Usitende jambo kwa kuwaangalia wanadamu wanasema nini bali Mungu anasema nini.
➽Tambua kwamba msaada juu ya kila unachokitenda haupatikani popote pale ila kwa Mungu pekee aliyekutuma.(usitafute msaada kwa wanadamu au kwa waganga au kwa miungu mingine)
➽Tambua kwamba mwajiri wako 'MUNGU' amekwisha kuandalia utaratibu mzima wa jinsi utakavyoish; chakula,malazi na makazi pia utaratibu wote wa maisha yako hapa duniani. Ndiyo maana anasema usisumukie kwamba utakula nini au utakunywa nini.
➽Tambua kwamba unapaswa kuwasiliana na Mwajiri wako kila wakati ili kumfahamisha kila kinachoendelea na njia pekee ya mawasiliano ni 'MAOMBI'
➽Tambua kwamba kuna mkataba ulioingia wewe na mwajiri wako, unapaswa uufate.
➽Tambua kuna mambo ambayo mwajiri wako amekwambia uyafuate pindi uwapo humu duniani na unapaswa ufuate (AMRI KUMI)
⧫Ni wakati wa kujitathimini kwamba upo wapi. je! umelala au umeamka? Je! upo kazini kuitenda kazi ya Bwana aliyokuitia hapa ulimwenguni au la?
⧫Katika chapisho linalokuja 'VOL....04' Tutaona uchambuzi zaidi wa Mkristo kuwa Balozi wa Mungu hapa ulimwenguni. hii ni sawa na utangulizi tuu wa somo litakalokuja karibu ujiunge nami katika kuliandaa kwa njia ya maombi ili Mungu aliwezeshe likawe na mafanikio makubwa kwa kila atakayesoma.ππππππππ
⭆Usiache kufuatilia masomo yaliyopita na masomo mbalimbali kwenye blog yangu hii.
⭆Share kwa wengine nao wapate kusoma na kufaidika kama wewe sasa.
⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲MUNGU AKUBARIKI SANA ⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲⇲
Mwandishi. Melchizedek Pokeaeli
➧ Unaweza kuyapata masomo mengine sehemu hizi zifuatazo
➢ christiansforum1.blogspot.com
Facebook: Joyful house in Jesus Christ
WhatsApp https://chat.whatsapp.com/CWsNX9vneY95rYMeuLNW9I
Twitter @johnsonpaulPAUL