Jumatano, 14 Machi 2018

TUTUNZE UUMBAJI

TUTUNZE UUMBAJI
Mwanzo 1:24-25

πŸŒ²πŸŒ³πŸŒ΄πŸŒΎπŸπŸ‘πŸ‹
Kwa harakaharaka KILA mmoja hakosi maana nzuri ya neno UUMBAJI.
Ila ukisoma mistari hiyo inaonyesha wazi kwamba vyote tunavyoviona; binadamu, wanyama, ndege, samaki, anga, jua, mwezi, nyota, milima ,mabonde, nk. Na vingine Vingi tusivyo viona vyote ni UUMBAJI._*
🌾 Watu wengi wanapokutana na neno =UUMBAJI= 🌿🌳🌴Huangalia mazingira yanayowazunguka pasipo kukumbuka hata wao wenyewe ni sehemu ya UUMBAJI Wa Mungu.
=>Tunaamini ya kwamba kwa siku Sita Mungu aliumba vyote vinavyoonekana na visivyooneka. Na baada ya kumaliza Mungu akaona vyote kuwa ni #Vyema
πŸšπŸžπŸ‹πŸπŸ΄πŸΊπŸπŸπŸ‘πŸπŸ‡πŸ€πŸŒΏπŸŒ΄πŸŒ²πŸŒ³πŸŒ•πŸŒΎπŸŒΉπŸŒŽ
✅soma Mwa.1:25b
Mungu akaona yakuwa ni vyema
Mwa.1:31
 "Mungu akaona KILA kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana..."
Swali ni kwamba kwanini sasaivi kuna chema na kibaya???!
πŸ†πŸŸ
πŸ‘‰πŸ‘‰ Embu tuendelee taratibu tutapata majibu..
"Wajibu Wa kwanza Wa Mwanadamu(Adamu&Hawa)"
Kutiisha,(kuitunza) na kutawala

✅ Soma MWA.1:28.
AHAA!! KUMBE
Mungu baada ya kuumba vyote na kuviona kuwa ni vyema alimkabidhi Mwanadamu wajibu Wa kuhakikisha uzuri Wa uumbaji haupotei.... Ohoo
Mwanadamu tokea hapo alikuwa responsible na KILA kinachoendelea kwenye UUMBAJI  Wa Mungu.!!!
πŸ˜ŠπŸ‘ΈπŸ‘‘: Mwanadamu akawa mtawala,  juu ya uumbaji.
"Maana ya mtawala ni kwamba hakuna kinachoweza kufanyika ndani ya himaya yake pasipo idhini yake. Yaani yeye kuridhia".
aha ndiyo maana hata kuwapa majina wanyama alifanya adamu na sio MTU mwingine
✅Soma Mwa.2:20b
πŸ₯πŸ΄πŸ—πŸΊπŸπŸœπŸžπŸ’πŸšπŸžπŸŸπŸ¬πŸ³πŸ‹πŸ†Kwasababu ya Mwanadamu Uumbaji ulibadilika. Wajibu Wa kwanza Wa Mwanadamu ni "Kuilima nchi" yaani kutiisha na kutawala.
πŸπŸπŸπŸ‚πŸ‚πŸ₯€πŸƒ☘πŸŒΏπŸŒ±πŸŒ΄πŸ€πŸ€πŸŒΎπŸŒΎπŸŽ‹πŸŒ³πŸŒ²πŸŽ„πŸŒ΅πŸ¦”πŸΏπŸ€πŸˆπŸ©πŸπŸ•

Mf. Wa uumbaji na Mwanadamu ni huu Wa kijana mmoja aliyekuwa anapendwa sana na Baba yake.

πŸ“‰Alipomaliza kidato cha nne, hakufaulu na ndipo Baba yake akamnunulia Bodaboda (Pikipiki) akamwambia Pikipiki hii nimenunia kwa gharama yangu lakini nakupa mwanangu Bure. Itunze na uitawale hii ni yako kwaajili ya kujipatia kipato na ada ya kuendelea na chuo.

Pikipiki ilikuwa mpya ila baada ya muda kidogo kijana yule anairudisha Pikipiki nyumbani ikiwa mbovu. Na baba yake anamwuliza KULIKONI!???

 Kijana huyo ndiye Mwanadamu. 
Mwanadamu ameshindwa kuutunza uumbaji Ambao Mungu amewapa kama Zawadi Toka kwake.

πŸŒΉπŸŒΉπŸŒΉπŸ’πŸŒΈπŸŒ·πŸŒΊ
Kumbe sio kwamba kupanda Maua au kupanda miti ndiyo kuitunza uumbaji la hasha. Ila kutenda yanayompendeza Mungu.
Kosa la Mwanadamu linakuwa pigo kwa viumbe wengine wote.
Kumbuka Misri. Ng'ombe, na viumbe wengine wote walipigwa kutokana na kugoma kwa farao kuwaruhusu Waisrael taifa la Mungu kwenda kumwabudu Mungu.

 ✅ soma Kut.12:12 (hukumu juu ya uumbaji wote Kyle Misri kutokana na dhambi ya farao/Mwanadamu) _"...nami nitawapiga wazaliwa Wa kwanza wote katika nchi ya Misri Wa Mwanadamu na Wa Mnyama, Nami jitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri"_

✅ Soma Law.18:20-23; 24-25, 27-28
πŸ‘†
Hapa tunaona jinsi dhambi ya zinaa inavyonajisi ardh.
Uasherati, utoaji mimba, na mahusiano ya jinsia moja nk.
Note.
JUU YA KUTUNZA. UUMBAJI  Mungu hazungumzii kuhusu Hewa safi/angavu , maji safi ila anahitaji *MAISHA SAFI*

πŸ‘‰  Unapotenda dhambi unaunajisi uumbaji Wa Mungu.
πŸ‘‰ Nayo Nchi itakutapika kama wenyeji Wa kanaani

HITIMISHO.
KUTUZA UUMBAJI SIO TUU KUPANDA MITI,MAUA NK. ILA NI KUISHI MAISHA YANAYO MPENDEZA MUNGU. ISHI MAISHA MEMA NA YANAYOMPENDEZA MUNGU NAWE UTAPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU NA KWENYE UUMBAJI WAKE. nawe utatawala na kuvitiisha vyote kama ilivyo mapenzi ya Mungu.

_Tafakari hii Imeandaliwa na Mtheologia Johnson Pokeaeli_

Fuatilia zaidi kwenye blog yangu
pokeaeli.blogspot.com
christiansforum1.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni