TUTUNZE UUMBAJI
Mwanzo 1:24-25
π²π³π΄πΎπππ
Kwa harakaharaka KILA mmoja hakosi maana nzuri ya neno UUMBAJI.
Ila ukisoma mistari hiyo inaonyesha wazi kwamba vyote tunavyoviona; binadamu, wanyama, ndege, samaki, anga, jua, mwezi, nyota, milima ,mabonde, nk. Na vingine Vingi tusivyo viona vyote ni UUMBAJI._*
πΎ Watu wengi wanapokutana na neno =UUMBAJI= πΏπ³π΄Huangalia mazingira yanayowazunguka pasipo kukumbuka hata wao wenyewe ni sehemu ya UUMBAJI Wa Mungu.
=>Tunaamini ya kwamba kwa siku Sita Mungu aliumba vyote vinavyoonekana na visivyooneka. Na baada ya kumaliza Mungu akaona vyote kuwa ni #Vyema
πππππ΄πΊπππππππΏπ΄π²π³ππΎπΉπ
✅soma Mwa.1:25b
Mungu akaona yakuwa ni vyema
Mwa.1:31
"Mungu akaona KILA kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana..."
Swali ni kwamba kwanini sasaivi kuna chema na kibaya???!
ππ
ππ Embu tuendelee taratibu tutapata majibu..
"Wajibu Wa kwanza Wa Mwanadamu(Adamu&Hawa)"
Kutiisha,(kuitunza) na kutawala
✅ Soma MWA.1:28.
AHAA!! KUMBE
Mungu baada ya kuumba vyote na kuviona kuwa ni vyema alimkabidhi Mwanadamu wajibu Wa kuhakikisha uzuri Wa uumbaji haupotei.... Ohoo
Mwanadamu tokea hapo alikuwa responsible na KILA kinachoendelea kwenye UUMBAJI Wa Mungu.!!!
ππΈπ: Mwanadamu akawa mtawala, juu ya uumbaji.
"Maana ya mtawala ni kwamba hakuna kinachoweza kufanyika ndani ya himaya yake pasipo idhini yake. Yaani yeye kuridhia".
aha ndiyo maana hata kuwapa majina wanyama alifanya adamu na sio MTU mwingine
✅Soma Mwa.2:20b
π₯π΄ππΊππππ’ππππ¬π³ππKwasababu ya Mwanadamu Uumbaji ulibadilika. Wajibu Wa kwanza Wa Mwanadamu ni "Kuilima nchi" yaani kutiisha na kutawala.
ππππππ₯π☘πΏπ±π΄πππΎπΎππ³π²ππ΅π¦πΏπππ©ππ
Mf. Wa uumbaji na Mwanadamu ni huu Wa kijana mmoja aliyekuwa anapendwa sana na Baba yake.
πAlipomaliza kidato cha nne, hakufaulu na ndipo Baba yake akamnunulia Bodaboda (Pikipiki) akamwambia Pikipiki hii nimenunia kwa gharama yangu lakini nakupa mwanangu Bure. Itunze na uitawale hii ni yako kwaajili ya kujipatia kipato na ada ya kuendelea na chuo.
Pikipiki ilikuwa mpya ila baada ya muda kidogo kijana yule anairudisha Pikipiki nyumbani ikiwa mbovu. Na baba yake anamwuliza KULIKONI!???
Kijana huyo ndiye Mwanadamu.
Mwanadamu ameshindwa kuutunza uumbaji Ambao Mungu amewapa kama Zawadi Toka kwake.
πΉπΉπΉππΈπ·πΊ
Kumbe sio kwamba kupanda Maua au kupanda miti ndiyo kuitunza uumbaji la hasha. Ila kutenda yanayompendeza Mungu.
Kosa la Mwanadamu linakuwa pigo kwa viumbe wengine wote.
Kumbuka Misri. Ng'ombe, na viumbe wengine wote walipigwa kutokana na kugoma kwa farao kuwaruhusu Waisrael taifa la Mungu kwenda kumwabudu Mungu.
✅ soma Kut.12:12 (hukumu juu ya uumbaji wote Kyle Misri kutokana na dhambi ya farao/Mwanadamu) _"...nami nitawapiga wazaliwa Wa kwanza wote katika nchi ya Misri Wa Mwanadamu na Wa Mnyama, Nami jitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri"_
✅ Soma Law.18:20-23; 24-25, 27-28
π
Hapa tunaona jinsi dhambi ya zinaa inavyonajisi ardh.
Uasherati, utoaji mimba, na mahusiano ya jinsia moja nk.
Note.
JUU YA KUTUNZA. UUMBAJI Mungu hazungumzii kuhusu Hewa safi/angavu , maji safi ila anahitaji *MAISHA SAFI*
π Unapotenda dhambi unaunajisi uumbaji Wa Mungu.
π Nayo Nchi itakutapika kama wenyeji Wa kanaani
HITIMISHO.
KUTUZA UUMBAJI SIO TUU KUPANDA MITI,MAUA NK. ILA NI KUISHI MAISHA YANAYO MPENDEZA MUNGU. ISHI MAISHA MEMA NA YANAYOMPENDEZA MUNGU NAWE UTAPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU NA KWENYE UUMBAJI WAKE. nawe utatawala na kuvitiisha vyote kama ilivyo mapenzi ya Mungu.
_Tafakari hii Imeandaliwa na Mtheologia Johnson Pokeaeli_
Fuatilia zaidi kwenye blog yangu
pokeaeli.blogspot.com
christiansforum1.blogspot.com