Ijumaa, 27 Aprili 2018

KANTANTE DOMINO. MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA ZAB.98

Zab.98
Maneno ya kwanza ya zaburi hii, kwa lugha ya kilatini yanamaana ya Cantate "Mwimbieni" (O sing) mwendelezo wake Cantate Domino -"Mwimbieni Bwana"
****************
Hii ni Siku ya pekee imefika ambayo tibaitumia katika kukumbushwa wajibu wetu kama wanadamu Kumsifu Mungu na kumtukuza yenye Peke Yake kwa ukombozi wake kwetu.
Wana Wa Israel walipotoka uhamishoni walimtukuza Mungu na kukwa kumwimbia nyimbo kuu za sifa. Kwa vinubi, zeze na kinanda. Walimsifu kwa kutimiza ahadi yake ya ukombozi. 2Nya.36:22-23).

Ahadi ya Mungu aliyoisema kwenye neno lake juu ya kuwa uhamishoni na kukombolewa kurudi kwenye nchi yao ya ahadi imetimia na sasa wanamtukuza.
Kwenye kitabu cha Kutoka.15 tunaona namna Musa na wana waisrael walivyomsifu Mungu kwa jinsi alivyowatoa utumwani.
Isa. 42:16 ...ni mwendelezo Wa ahadi ambayo hata sasa tunaiona imetimia kwa Yesu Kristo. Kutufia msalabani na kufufuka kwaajili ya wokovu wetu.
Tunayobudi kumsifu Mungu kwa Upendo wake kwetu.

Wengine wanauliza nitawezaje kusifu wakati nipo kwenye shida na majonzi.
Mungu anasema anakaa juu ya sifa za watu wake. Hii inatupa uhakika kwamba katikati ya Sifa Mungu anashuka na kushughulika na mahitaji yetu. Wengine wagonjwa wengine wana dhiki kuu. Sio mpaka uwekewe mikono ila kupitia sifa na kumwabudu Mungu basi yeye Mungu,hushuka na kutuponya.

Kuanzia Leo badili mtazamo wako kuu ya kusifu kwamba ni wakati Wa furaha tu! LA wakati ule unapokuwa huwezi kabisa na upo katikati ya dhiki kuu, vifungo vimekuandama mawazo yamekuwa mengi, huoni njia, ukiomba Maneno yanayotoka ni ya kulaumu tu. Huo ndiyo wakati Wa kumwimbia Bwana wimbo mpya.
Wimbo mpya huleta matumaini ya Wokovu. Matumaini ya kuwa huru tena. Kama ulikuwa umeanguka unapata matumaini ya kuinuka na kusonga mbele. Kama ulikuwa firisika matumaini ya kuwa tajiri tena. Kama ulifukuzwa kazi unapata matumaini ya kurejea kazini tena, kama huna Mtoto unapata matumaini ya kupata watoto. Huna Mume/Mke, familia inaugomvi, watoto hakutii. Katikati ya kumsifu Bwana Unaona kuinuka na kuang'aa tena .
Hitimisho.
Paulo na sila wakamsifu Mungu hadi pingu zika katika. Na milango ya Gereza ikafunguka.
Nawe msifu Mungu sasa utapokea Majibu ya Mungu juu uhitaji ulio nao.
Amen!!
pokeaeli.blogspot.com
christiansforum1.blogspot.com